Halmashauri ya Wilaya ya Same kupitia Kitengo Cha Manunuzi Serikalini kimeendelea kutoa Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa kielekroniki wa manunuzi ya Umma (NeST) kwa makundi mbalimbali ya watumishi ili kuwawezesha kutumia Mfumo huo kila wanapofanya manunuzi ya Umma.
Afisa Manunuzi wa Wilaya ya Same Bw.Rashid Kimweri amesema kuwa mafunzo hayo yameshatolewa kwa wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya na kwasasa wanatumia vema mfumo huo kufanya manunuzi.
"Ni maelekezo ya Serikali kuwa Manunuzi yote ya Umma yafanyike kupitia Mfumo wa NeST na kwakuwa huu mfumo bado watumishi hawajauzoea tunaendelea kutoa mafunzo ili kuhakikisha watumishi wote wanakuwa na uwezo mzuri wa kutumia mfumo huu " alisema Kimweri.
Aliyataja makundi mengine ambayo yameshapatiwa mafunzo hayo kuwa ni waganga viongozi wa vituo vya Afya na Hospitali na zahanati na kwasasa mafunzo hayo yametolewa kwa walimu wakuu na walimu wa manunuzi.
Akitoa Mafunzo kwa Walimu Ugavi Wilayani Same Bw.Francis Yona alisema ni lazima manunuzi yote ya Serikali yafanyike kupitia NeST hivyo akawataka walimu hao kuwa na usikivu muda wote wa mafunzo ili waweze kwenda kufanya manunuzi kupitia mfumo.
Alisema Miradi inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Same ni mingi hivyo wasimamizi wote wa Miradi wanapaswa kujua kutumia Mfumo huu.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.