Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama leo Agosti 16,2024 amebandika Tangazo la mipaka na majina ya Vijiji na Vitongoji ikiwa ni sehemu ya Maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Nov 27 mwaka huu.
Akibadika Tangazo hilo mbele ya Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Upendo Wella na Afisa Uchaguzi (W)Bw.Yohana Peter, Mkurugenzi alihimiza wananchi wote kusoma Tangazo hilo ili waweze kufaham mipaka ya maeneo yao.
"Leo Tangazo hili nimelibandika hapa Ofisi za Halmashauri lakini pia watendaji wa Kata wameshapewa kwaajili ya kubandika kwenye maeneo ya Vijiji"alisema Mhagama
Nae Katibu Tawala wa Wilaya Bi.Wella aliwataka watendaji kuhakikisha kuwa matangazo hayo yanabandikwa kwenye maeneo yao ili wananchi waweze kuyasoma.
"Pamoja na matangazo haya lakini kaelimisheni wananchi kuwa kila mmoja atapiga kura kwenye Kitongoji alichojiandikishia"amesema Bi. Wella
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini unatarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.