Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi Bw.Jimson Mhagama amesema tayari Viongozi wa Serikali za Vijiji 100 ambavyo vinaundwa na vitongoji 503 wameapishwa viapo vya uaminifu na kutunza siri pamoja na kiapo cha utii na uadilifu.
Bw.Mhagama amesema zoezi la uapishaji limefanyika Novemba 28 kwenye vituo saba tofauti vya uapishaji ili kuwarahisishia viongozi hao kufika kwenye meneo hayo kirahisi.
“Tayari Wenyeviti wetu wa Vijiji,Vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za vijiji wameapishwa ambapo idadi yao inafikia 2500, uapishwaji huu umekwenda sambamba na utoaji wa semina elekezi kwa viongozi hao”
Msimamizi huyo wa Uchaguzi alisema baada ya kuapishwa sasa viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuanza utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi katika masuala mbalimbali.
Akizungumza baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbakweni Kata ya Msindo Bw.Tuarira Mmbaga aliwashukuru wananchi wa kijiji chake kwa kumuamini na kumchagua.
“Nimefurahi kuapishwa leo, niwaahidi tu wananchi wa Mbakweni kwamba sasa tunakwenda kuanza kazi ya kuhakikisha kwamba kijiji chetu kinasonga mbele kwa maendeleo” alisema
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.