Wananchi wa Wilaya ya Same wameshauriwa kupima ugonjwa wa ini ili waweze kupatiwa chanjo mapema ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa ini ili kunusuru maisha yao.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mheshimiwa Yusto Mapande kwenye kikao cha Baraza la Madiwani ambapo aliwataka Madiwani kufikisha ujumbe huo kwa wananchi ili waweze kulinda afya zao.
“Ndugu zangu Madiwani nyie ni viongozi wa karibu na wananchi, hivyo mna jukumu kubwa la kuwahamasisha kupima afya zao, hasa kwa magonjwa hatari kama ini ambayo kama mtu hajapata maambukizi anapatiwa chanjo ya kumlinda na maambukizi" alisema Mheshimiwa Mapande.
Dkt. Alex Alexander, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, alieleza kuwa ugonjwa wa ini ni miongoni mwa magonjwa hatari na unahitaji juhudi za pamoja katika kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kupima mapema na kupata kings.
“Tunawashauri wananchi kupima ugonjwa huu mapema kwani mara nyingi dalili zake huonekana katika hatua za mwisho, hivyo ni muhimu wananchi kupima mapema ili kupata kinga” alisema Mganga Mkuu wa Wilaya.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, ugonjwa wa ini unaweza kuzuilika kwa chanjo, lishe bora, na kuepuka matumizi ya pombe kupita kiasi.
Halmashauri hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha huduma za upimaji na matibabu ya ugonjwa huo kwa wananchi wa Same
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.