NGO ya EMPOWER TANZANIA imekabidhi jengo la kituo kinachotoa huduma kwa mama na mtoto kilichopo kitongoji cha Nadururu kata ya Maore baada ya kukiendesha kwa miaka 6.Pia wamekabidhi baiskeli 69 kwa watoa huduma ya msingi wilayani.Taasisi hii imekuwa ikifanya kazi wilaya ya Same katika maeneo ya afya,elimu,mazingira na wameahidi kuleta mradi wa maji kijijini hapo.
Vyeti walivyotoa kwa wakunga wa jadi vimekuwa ni kivutio kwa jamii hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa kupinga ukeketaji na kutoa ushauri kwa wakinamama kujenga tabia ya kupata huduma za hospitali.
Rais wa NGO hiyo Bi.Joddy Morgan toka lowa Marekani ameahidi kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Same;ambapo Mkurugenzi wa NGO hiyo Ndg.Elibariki Kisimbo ametoa taarifa ya uanzishaji wa mradi mpya wa elimu ya afya na stadi za maisha mashuleni ili kuunga mkono juhudi za wilaya za kupambana na mimba kwa wanafunzi.Pia walitoa neti 500 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.
DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule akiwashukuru alisema"Kazi hii inafanya wilaya kupunguza vifo vya mama na mtoto,naagiza Halmashauri kuhakikisha kituo hiki kinaendelea kutoa huduma".Awashukuru kwa kutaka waendelee kuwa walezi wa kitongoji hicho kama wananchi walivyoomba.Awataka waliopewa baiskeli kuzitunza na kuzitumia kama zilivyokusudiwa.
"Same is not same"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.