Katibu Tawala Wilaya ya Same Bi.Upendo Wella leo ameongoza watumishi wa Serikali pamoja na wananchi wilayani Same kwenye zoezi la kufanya usafi katika kituo kikuu cha mabasi Wilaya ya Same katika kuadhimisha siku ya Mashujaa inayofanyika Julai 25 ya kila mwaka.
Maadhimisho ya siku ya Mashujaa kitaifa mwaka huu yamefanyika Dodoma katika Makao Makuu ya Taifa ,hivyo Taifa limetenga siku hii rasmi kwaajili ya kuwakumbuka Mashujaa waliopambana kuhakikisha wanakomboa Taifa letu la Tanzania.
Akizungumza na wafanyabiashara pamoja na wananchi alisema siku ya Mashujaa ni muhimu kwa inatumika kuwakumbuka Mashujaa ambao walipambania Taifa hivyo ni vyema kufanya shughuli mbalimbali za kijamii .
"Tumekuja kufanya usafi hapa kituo cha mabasi Same kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mashujaa kama tunavyofahamu kwamba siku hii ni siku mahususi kwaajili ya kuwakumbuka Mashujaa wetu ambao walifanya shughuli mbalimbali za kulitetea Taifa letu na kuleta maendeleo” amesema
Katibu Tawala alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha wananchi pamoja na wafanyabiashara kwamba Jambo la kufanya usafi ni jukumu lao katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakua safi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama naye pia ameshiriki kwenye zoezi la kufanya usafi ambapo aliwahamasisha wafanyabiashara wote kuhakikisha wanafanya usafi kwenye maoneo yao ya kazi.
"Siku ya leo Julai 25 kwenye nchi yetu tunaadhimisha siku ya Mashujaa, Halmashauri yetu ya Same tumefanya usafi kwahiyo tutaendelea kusimamia suala la usafi ,wafanyabiashara wanapaswa kuhakikisha eneo lao la biashara lipo safi na wasipozingatia hilo tutatumia sheria zetu ndogo kuwapiga faini"amesema Mhagama
Kaimu Afisa Afya Wilaya Bw.Moses Timotheo amewashukuru wananchi wote pamoja na viongozi waliojitokeza kwenye zoezi la kufanya usafi kwani kitendo hicho kinajenga tabia za usafi pamoja na kuepusha kutapakaa kwa takataka na hivyo kulinda afya zao.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.