Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amewataka wananchi wote wenye sifa za uongozi kuchukua fomu kwaajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa alitoa wito huo alipotembelea Wilaya ya Same ambapo alisema zoezi la uandikishaji wapigakura limeshamalizika na baada ya majina ya wapiga kura kuhakikiwa kitakachofuata ni kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
“Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa na Mwenyekiti wa Kitongoji pamoja na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji zitaanza kutolewa rasmi Oktoba 26 hadi Novemba 1, 2024” Alisema Mheshimiwa Babu.
Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wote wenye sifa kuchukua fomu kwaajili ya kugombea nafasi hizo ili Vijiji na Mitaa viweze kupata viongozi bora.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Same Mashariki na Same Magharibi Bw.Jimsoni Mhagama alizitaja sifa za kugombea nafasi hizo ni kuwa raia wa Tanzania na Mkazi wa Kijiji au Kitongoji husika,kuwa na umri wa kuanzia miaka 21 na kuendelea,ajue kusoma na kuandika Kiswahili au kiingereza,awe na shughuli halali ya kumuwezesha kuishi na awe mwanachama wa chama cha siasa na awe amedhaminiwa na chama chake kugombea.
Amesema kwa yeyote mwenye sifa zilizotajwa ana haki ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Jumla ya vijiji 100 na Vitongoji 503 vya wilaya ya Same vinatarajia kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.