Wananchi wa Kata ya Ruvu wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe.Yaigongo Mrutu wameiomba Serikali kuwapatia chakula cha msaada kwani mazao yaliyokuwa shamba yameathiriwa na mafuriko hivyo kuwaacha bila chakula.
Akizungumza na wananchi hao ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amewaahidi kuwa Serikali itawapatia chakula cha Msaada ili waweze kuvuka kwenye changamoto hiyo.
"Serikali haiwezi kuacha wananchi wake wafe kwa kukosa chakula,tayari tumeshapokea taarifa toka kwa Mkuu wa Wilaya kwamba watu wa RUVU mmepata janga la njaa na tumeshawasilisha maombi Ofisi ya Waziri Mkuu hivyo mtapatiwa chakula cha msaada"alisema Mheshimiwa Babu.
Mkuu wa Mkoa amefanya ziara ya siku moja Wilayani Same ambapo akitembelea Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya (Ruvu),Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya (Kirinjiko),Ujenzi wa Bwalo la Chakula (Sekondari ya Kibacha) na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Angellah Kairuki (Kisima).
Akiwa Wilayani Same Mkuu wa Mkoa aliwapongeza viongozi wa wilaya hiyo kwa usimamizi nzuri wa Miradi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.