Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya Lenana Holdings Ltd anayejenga daraja la Makanya Estate kuhakikisha kuwa anakamilisha ujenzi huo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu kama ilivyo kwenye matakwa ya mkataba.
Mkuu wa Mkoa alitoa agizo hilo alipotembelea kukagua na kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo linalounganisha Kata ya Makanya na Suji.
“Mkandarasi hakikisha kwamba daraja hili linakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye makubaliano ili kurejesha mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wa Kata za milimani na maeneo mengine” alisema Mkuu wa Mkoa.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa,Meneja wa TARURA Wilaya ya Same Mhandisi James Mnene alisema fedha zilizopokelewa kwaajili ya ujenzi daraja hilo la mawe lenye urefu wa Mita 46 ni shilingi milioni 410 lakini mkandarasi alipatikana kwa shilingi milioni 399.
Alisema ujenzi huo ulitarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu lakini ilishindikana kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha hivyo mkandarasi aliongezewa muda hadi mwisho mwa mwezi Mei mwaka huu.
Nae Mwakilishi wa Kampuni ya Lenana holding Ltd Bw.Ally Tesha alimuahidi Mkuu wa Mkoa kukamilisha ujenzi huo mwsihoni mwa mwezi Mei 2024.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.