Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu ameliagiza jeshi la polisi Wilaya ya Same kuhakikisha wanawasaka na kuwakamata watu wanaoharibu samani kwenye eneo la kumpumzikia watu wanaopanda Mlima Shengena.
Mheshimiwa Babu ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara kwenye eneo Hilo ambapo alishuhudia uharibifu mkubwa ukiwa umefanyika eneo hilo.
"Serikali inatumia pesa nyingi kutengeneza hivi vitu ili watalii wanaopanda Mlima Shengena wapate sehemu ya kupumzikia wanaposhuka lakini wahuni wachache wanaviharibu,hii haivumiliki,jeshi la polisi hakikisheni wahusika wanakamatwa"alisema Mkuu wa Mkoa
Awali akitoa taarifa ya tukio hilo Mhifadhi wa Msitu wa Asili Chome (Shengena) Bw.Yusuf Kajia alisema tukio hilo la kuvunja viti cha kupumzikia imetokea Kwa mara ya pili.
Mwaka jana walivunja pia na mwaka huu wamekuja tena wamevunja,hali hii inatupa wakati mgumu sana maana gharama ya ukarabati ni kubwa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amefanya ziara ya siku moja Wilayani Same ambapo alitembelea Miradi ya TASAF na Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Milima ya Tao la Mashariki ambapo hifadhi ya Chome imetekeleza Mradi wa upandaji miti.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.