Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Kiseo Nzowa amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni kwa maandalizi mazuri ya Tamasha la Same Utalii Festival.
Ametoa pongezi hizo wakati akizindua Tamasha hilo la siku tatu lililoanza leo ambapo alisema pamoja na Tamasha hilo kutangaza Utalii lakini pia ni chachu ya Maendeleo Wilayani himo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu, Katibu Tawala Bw. Nzowa, alisema kuwa tamasha hilo pia ni kituo cha uwekezaji.
Amesema kuwa, mbali na kutangaza vivutio vya utalii, tamasha hili limeongeza mzunguko wa biashara pale wageni wanapofika wilayani Same.
"Tamasha hili la Same Utalii Festival linasaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Same, na pia limeweza kutambua rasmi vivutio hivyo kama mali kale na maeneo ya utalii," alisema Nzowa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni, amesema kuwa lengo la tamasha hili ni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kutangaza utalii kupitia Filamu ya Royal Tour, ambayo imeleta mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya watalii nchini.
Kasilda alisisitiza kuwa, lengo jingine ni kuhakikisha kuwa vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Same vinawanufaisha wananchi wa wilaya hiyo, pamoja na kuhamasisha uwekezaji kupitia sekta ya utalii.
"Moja ya mafanikio makubwa tuliyoyapata kupitia awamu ya kwanza ni kuweza kupata wawekezaji watatu ambao wanajenga hoteli za kisasa tatu wilayani Same, jambo litakalosaidia kutoa ajira kwa vijana," alisema Kasilda.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya utalii vya Same imeongezeka mara mbili, na hivyo kuchangia kukuza vipato vya wananchi wa Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.