Mamlaka ya Mji Mdogo Same imemchagua Bw.Ramadhani Mangare kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ambaye ataongoza Mamlaka kwa kipindi cha miaka mitano huku Bi.Theopista Merdad akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Katika Uchaguzi huo uliofanyika Januari 21,2025 Jumla ya wajumbe 21 walipiga kura ambapo kura za ndio zilikuwa 20 na hivyo kuwapa ushindi wagombea hao.
Bw.Mangare aliwashukuru wajumbe kwa kumuamini na hivyo kuahidi kusimamia vema Miradi ya Maendeleo pamoja na Usimamizi mzuri wa mapato.
"Katika kipindi changu cha Uongozi nitaweka kipaumbele kwenye kutembelea Miradi,kuhamasisha uwekezaji na kusimamia Utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Mamlaka"alisema.
Mwenyekiti huyo pia aliahidi kushirikiana na watumishi wa Mamlaka kuboresha sekta mbalimbali ili kufikia lengo la kuwa Mji kamili ifikapo 2030.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maendeleo kwenye Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo Same Bw.Lusasi Uledi alisema kwa mwaka 2024/25 Mamlaka imelenga kukusanya Mil.300.4 na tayari wameshakusanya zaidi ya asilimia 62.
Alisema Mamlaka pia inatekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Ujenzi wa Bweni na Bwalo la chakula Shule ya Sekondari Kibacha,Ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi Majevu.
Aliitaja Miradi mingine kuwa ni Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu (2 in 1) Shule ya Sekondari Angellah Kairuki na ukarabati wa Zahanati ya Masandare ambao umeshakamilika ambapo Miradi Mingine ipo hatua za umaliziaji.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.