Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mhe.Yusto Mapande amepongeza usimamizi wa utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Madarasa na matundu ya vyoo unaotekelezwa na Mradi wa BOOST katika Wilaya ya Same.
Mhe. Mapande ametoa pongezi hizo wakati Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ilipotembelea na kukagua miradi ya BOOST inayotekelezwa katika shule 10 za Msingi ambayo inagharimu shilingi bil. 1.8.
Mwenyekiti amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Anastazia Tutuba pamoja na timu yake ya Wataalam kwa usimamizi mzuri wa Miradi hiyo kwani imejengwa kwa kiwango kinachostahili na thamani ya fedha imeweza kuonekana" Mmefanya kazi nzuri, kazi inavutia, inafaa kuonyeshwa kwa kila mtu naye atatamani kujifunza kutoka kwenu"amesema Mhe.Mapande.
Mradi wa BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Same unajenga shule mbili mpya za msingi ambazo ni Kisima na Mgandu pamoja na madarasa thelathini na nne (34) katika shule nane (8) za msingi pamoja na matundu ya vyoo.
Shule nane zilizonufaika na ujenzi wa madarasa ni Mbono na Ndolwa ambazo kila moja imepata madarasa saba,Kwesasu,Turiani na Mpirani kila moja madarasa matano,Kikwete madarasa sita,Dimwi madasrasa matatu na Mbuyuni madarasa mawili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuwaletea miradi mbalimbali hususani kwenye sekta ya Elimu ambapo imesaidia kupunguza tatizo la upungufu wa madarasa kwa wanafunzi pamoja na kuepusha wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.
"Tumepokea fedha nyingi za miradi tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Same” amesema Bi.Tutuba.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgandu inapojengwa shule mpya ya Msingi, Bw. Amiri Dongo amemwomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi. Anastazia Tutuba kumsaidia kupata waalimu wenye uweledi wa kufundisha ambao watasaidia shule hiyo kuwa na ufaulu mzuri.
Pia Diwani wa Kata ya Bendera Mhe. Mhina Mmasa ameishukuru Serikali kwa kuwapatia Mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya kwani itasaidia kupunguza changamoto ya umbali kwa wanafunzi kwenda shuleni kwani walikuwa wanaenda kusoma Kata ya jirani ambapo ni mbali.
"Ujenzi wa shule hii umepunguza changamoto kwa sababu watoto walikuwa wanasoma mbali ambapo wakati wa mafuriko wanakaa hadi mwezi bila kufika shuleni kwani daraja wanalolitegemea kuvuka hujaa maji” amesema Mhe.Mmasa.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.