Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu amekabidhi Mwenge wa Uhuru 2024 kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani.
Mwenge wa Uhuru 2024 uliwashwa Kitaifa Mkoani Kilimanjaro April 2,2024 na kukimbizwa katika Halmashauri Saba za Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwenge wa Uhuru ulianzia Mbio zake kwenye Manispaa ya Moshi April 2 na kumalizia Mbio zake kwenye Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Ukiwa Mkoani Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru ulitembelea,kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi 47 yenye thamani ya Shilingi Bil.29.3.
Akitoa ujumbe wa Mwenge katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava alihimiza wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao anatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.
"Wananchi tujitokeze kugombea na kupiga kura lakini pia tuhakikishe tunachagua viongozi bora kwa Maendeleo ya Taifa letu" alisema Ndg Mnzava.
Ndg. Mnzava ambaye aliotesha miti katika Miradi yote aliyotembelea mkoani hapa pia alihimiza utunzaji wa Mazingira pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizindua klabu ya wapinga rushwa kwenye Shule ya Sekondari Makanya Wilayani Same Ndg. Mnzava alikemea vikali tabia ya kuomba na kutoa rushwa.
"Sote tunatambua kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo kila mtu ahakikishe anapiga vita vitendo vya rushwa ili tuwe na Taifa la watu wenye uadilifu"alisema.
Aidha katika ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa hatari WA UKIMWI.
"Ndugu zangu UKIMWI upo na unaendelea kuua hivyo tuchukue tahadhari na kwa wale wanaotumia dawa za kufubaza makali ya UKIMWI wazingatie maelekezo"alisema Ndg Mnzava.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na Mbio zake mkoani Tanga na unatarajiwa kukimbizwa kwa siku 195 Tanzania Bara na Visiwani chini ya Kaulimbiu isemayo "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.