Ofisi ya Mkuu wa Willaya ya Same kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same wanayo furaha kuwakaribisha katika hafla ya mapokezi ya mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru 2021.
Wilaya ya Same inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 05/06/2021 ukitokea Mkoa wa Tanga.Eneo la mapokezi ni viwanja vya shule ya Msingi Chekereni iliyopo kata ya Mabilioni umbali kilometa 74 kutoka Same mjini.
Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 utatembelea jumla ya miradi saba(7);
Hali ya hewa ya wilaya ya
Same wakati wa asubuhi na usiku kuna hali ya baridi na upepo kiasi,unashauriwa kuwa na nguo za baridi ambazo si nzito sana.Pia unashauriwa kutumia kinywaji murua cha Tangawizi.Malazi ,chakula na vinywaji tunazo Hoteli zifuatazo;
Nzoroko Hotel World ni hoteli nzuri yenye mazingira ya kuvutia na mazingira yake ni masafi yakipendezeshwa na miti mizuri iliyostawishwa kwa ustadi mkubwa ,ukiwa Nzoroko utapata huduma za chakula,malazi,michezo mbalimbali na free wifi kwa mawasiliano.KM 74 kwenda eneo la mapokezi.0763599390.
Elephant Motel ni hoteli yenye mazingira mazuri na miti ya kupendeza na free wifi zinapatikana ukiwa hapo.Ipo KM 71 kwenda eneo la mapokezi ya Mwenge.Mawasiliano 0784499065
Yassir Hotel inatoa huduma bora na ipo pembezoni mwa barabara kuu jirani na kituo cha Polisi Same na huduma zote zinapatikana.Ipo KM 74 kwenda eneo la mapokezi.Mawasiliano 0719795599
Josonvilla Hotel ni hoteli nzuri yenye mazingira ya kuvutia na huduma zote zinapatikana,utapata wasaa wa kuogelea kwenye swimming pull na pia kuna free wi-fi,abundance of good creation,scenic beauty.Hoteli ipo Same mjini kitongoji cha stelingi.Kutoka hapo kwenda Chekereni ni kilometa 72 kwenda eneo la mapokezi Chekereni.Mawasiliano 0784499065.
Hedaru Palace Hotel ni hoteli nzuri ya kisasa iliyopo Hedaru na huduma nyingi zinapatikana.Umbali kutoka Hedaru kwenda eneo la mapokezi inakadiriwa kufikia KM 14 kwa mawasiliano 0621005425
Mwambashi Hotel ni hoteli nzuri iliyopo Hedaru na huduma zote nzuri zinapatikana.Umbali kutoka Hedaru kwenda eneo la mapokezi inakadiriwa kufikia KM 14.Kwa mawasiliano 0712102000.
Sunset Lodge ni eneo zuri kwa mapumziko na bei yake ni nafuu.Hoteli ipo Hedaru umbali kufikia eneo la mapokezi inakadiriwa kuwa KM14.Mawasiliano 0622677869.
Tunawakaribisha sana.
Same is not the same.
Mwenge wa Uhuru 2021 Oyeeeeeeee!!!!
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.