Vyama vya siasa ambavyo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi mdogo wa marudio Wilayani Same vimetakiwa kutangaza Sera na sio kujenga mfarakano miongoni mwa wananchi.
Akizungumza na viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo,Msimamizi wa Uchaguzi Wilayani humo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Bi.Anastazia Tutuba amewataka Viongozi hao kuzingatia maadili ya Uchaguzi katika kipindi chote Cha Kampeni.
"Kampeni zote zinazofanyika zilenge kutangaza sera za vyama husika yaani tujikite zaidi katika kuwaeleza wananchi kwamba watanuafaika vipi kwa kuchagua chama chako na sio kufanya siasa za chuki,kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi"alisema Bi.Tutuba.
Msimamizi huyo pia alionya vyama vya siasa kutofanya kampeni katika majengo ya Ibada wala kutumia viongozi wa dini katika kutangaza sera zao.
Wilaya ya Same inatarajia kufanya Uchaguzi wa marudio katika Kata za Njoro (Same Magharibi) na Kalemawe (Same Mashariki) Julai 13 mwaka huu kutokana na vifo vya waliokuwa Madiwani wa Kata hizo
Kampeni za Uchaguzi zimeanza Julai 1 na zitamalizika Julai 12 mwaka huu ambapo jumla ya wagombea nane wanatarajia kuchuana.
Afisa Uchaguzi Wilaya ya Same Bw.Yohana Peter aliwataja waliopitishwa kugombea Udiwani katika Kata ya Njoro kuwa ni Omar Abeid Abdalah (CCM),Raphael Mbonea Mrutu (NCCR-Mageuzi),Kasimu Rashid Msuya (ADC) na Paulo Juma Mshana (TLP) ambapo mgombea wa CHADEMA Dainel Onesmo Mziray alijiondoa baada ya kukosa wadhamini.
Katika Kata ya Kalemawe wapo wagombea watatu ambao ni Musa Hendrish Filipo (CUF),Jofrey Mtwa Jofrey (CCM) na Helena Juma (TLP) na mgombea wa CHADEMA Rajabu Kilango Bushiri alijiondoa kwa kukosa wadhamini.
Kata hizo zinarudia uchaguzi kutokana na kufariki kwa Diwani Athumani Mbelwa aliyekiwa Diwani wa Kata ya Kalemawe na Diwani Clement Mchomvu aliyekuwa Diwani wa Kata ya Njoro.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.