Wilaya ya Same imepokea Shilingi Milioni 402.7 kutoka Miradi wa SWASH kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi ya huduma za maji na Usafi wa Mazingira Vijijini-SRWSSP ambapo fedha hizo zimenufaisha jumla ya Zahanati 10 Wilayani humo.
Akizungumzia Miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Be.Jimson Mhagama amesema fedha hizo zimepokelewa kwa awamu tatu mfululizo.
Amesema awamu ya kwanza Wilaya ilipokea Shilingi Mil.160.7 ambazo zilinufaisha Zahanati nne na awamu ya pili zilipokelewa Shilingi Mil.200 ambazo zilinufaisha Zahanati tano.
"Awamu ya tatu tumepokea milioni 42 ambazo zimeelekezwa kujenga miundombinu ya maji na Usafi wa Mazingira kwenye Zahanati ya Mbakweni"alisema Bw.Mhagama.
Akitoa mchanganuo kuhusu matumizi ya fedha hizo Afisa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wilaya ya Same Bi.Yuster Malisa alisema fedha zilizotolewa awamu ya kwanza zilitumika kwenye Zahanati nne ambapo kila Zahanati ilijengewa vyoo,mnara wa kuweka tenki la maji,kichomea taka (incenereta) ,vinawia mikono na shimo la majivu na kutupa kondo la nyuma la mama.
"Awamu hii ilinufaisha Zahanati za Masandare,Makanya Kitivo,Kitivo na Ruvu Kombo"alifafanua Bi.Malisa na kuongeza kuwa Zahanati zilizonufaika awamu ya pili kuwa ni Kadando, Kihurio, Kasapo, Suji Malindi na Saweni.
Amesema kuwa katika awamu ya tatu ambapo Wilaya imepokea Mil.42 zilielekezwa Zahanati ya Mbakweni ambapo imetumika kujenga vyoo, kichomea taka, mnara wa tenki la maji,shimo la kutupa majivu na la kutupa kondo la nyuma.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.