Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa zoezi lililoanza leo la Undikishaji wananchi kwenye Daftari la Mkazi.
Akizungumza baada ya kujiandikisha kwenye kituo cha Stesheni na kutembelea baadhi ya Vituo, Mkuu wa Wilaya alisema zoezi hilo linaendelea vizuri kwani wananchi wamejitokeza kwa wingi.
"Kwakweli mwamko ni mzuri maana wananchi wamehamasika vituo vingi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha na bado wanaendelea kujitokeza"alisema.
Mheshimiwa Kasilda amesema Wilaya ya Same inatarajia kutumia vema siku kumi za uandikishaji ili kuweza kuandikisha wakazi 108,423.
"Mimi tayari nimejiandikisha, lakini pia nimepata nafasi ya kukagua baadhi ya vituo kuona hili zoezi linaendaje, nimefarijika sana zoezi linaendelea vizuri wananchi wamehamasika vituo vingi wameshajiandikisha na bado wanaendelea kujiandikisha”. Alisema Mhe. Kasilda.
Zoezi la uandikishaji wapigakura kwenye daftari la Mkazi limeanza leo Oktoba 11 nanlinatarajia kukamilika Oktoba 20 mwaka huu.
Wilaya ya Same ina Jumla ya Vituo 503 vya uandikishaji ,vilivyo ndani ya Vijiji 100 na Kata 34.
Zoezi la Uandikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi limeanza rasmi leo Oktoba 11 na linaendelea hadi kufikia Oktoba 20 mwaka huu 2024.
Kauli mbiu “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.