Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Jonas Mpogolo amewataka Watendaji ngazi ya Halmashauri,kata na vijiji kutekeleza afua za lishe ili kuwa na jamii yenye afya bora kwa ustawi wa Same na Taifa la Tanzania kwa ujumla.Akizungumza katika kikao hicho amewaasa watendaji kushirikiana kwa karibu na watoa huduma katika jamii kwa kuwa watoa huduma hao ndio wanahusika moja kwa moja katika maswala ya lishe kwa wananchi.
Aidha Mhe.Edward Jonas Mpogolo amewaagiza watendaji wa kata kuchukua tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia viongozi wa dini,wito wa mikutano katika kila kata na kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuvaa barakoa pindi wanapokuwa kwenye mikusanyiko.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.