Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni ,amewapongeza wadau wa elimu kutoka shule mbalimbali zinazomilikiwa na serikali,watu binafsi na mashirika ya dini zilizofanya kwenye matokeo ya mitihani ya Taifa mwaka jana.
Mhe. Kasilda ameeleza kufurahishwa na uboreshaji wa elimu kwenye shule hizo ambazo zimefanya vizuri, pia amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili shule hizo ziendelee kufanya vizuri zaidi.
“ Serikali tutaendelea kutoa ushirikiano ili muweze kufanya vizuri zaidi kwenye elimu,lakini pamoja na pongezi hizi ninaomba sana zile changamoto ambazo zinasababisha wanafunzi kutofanya vizuri mkazifanyie kazi kwani lengo kuu la kikao hichi cha elimu ni kuhakikisha ufaulu unaongezeka”alisema
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Same Mwl.Marclaud Mero alisema wilaya ya Same ina jumla ya shule za Msingi za Serikali 188 na za binafsi 18 hivyo kufanya jumla ya shule za msingi 206, shule za Sekondari zipo 66 kati ya hizo 46 ni za Serikali na 20 ni za sekta binafsi na chuo cha Ualimu kimoja ambacho kipo chini ya dini.
“Kikao hiki cha wadau wa elimu ni cha muhimu katika kutathimini maendeleo ya elimu na kutathimini matokeo ya mitihani iliyopita hivyo mnapaswa kushiriki kikamilifu katika kuandaa mikakati ambayo itasaidia kuinua taaluma na ufaulu katika Halmashauri yetu” alisema Mwl.Mero.
Kwa upande wake Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Same Bw. Godfrey Sebulu amesema “kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Utumishi wa walimu ya mwaka 2016 inawatambua wakuu wa shule ndio wenye mamlaka kamili ya usimamizi wa maadili ngazi ya shule hivyo wanapaswa kuwasimamia kikamilifu walimu walio chini yao”
Mthibiti Ubora wa Elimu Wilaya ya Same Bw.Calist Youze alisema suala la ufaulu wa wanafunzi linahusisha Serikali, walimu ,wanafunzi na wazazi,hivyo kila mmoja anapaswa kusimama kwenye nafasi yake.
Hata hivyo kikao hicho kiliazimia kuwasuala la nidhamu na maadili ya mwanafunzi yaanzie kwa wazazi,kuwe na ushirikiano mzuri katika swala taaluma kati ya walimu na wazazi, walimu watumie mbinu mbalimbali kuwajengea wanafunzi mazoea ya kujisomea, kila siku wanafunzi wapewe maswali ya Hesabu ili kuongeza ufaulu kwenye somo la Hisabati.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.