Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni amewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi ambayo hupata athari za Mafuriko au maporomoko ya miamba (landslides) kuhama maeneo hayo kwa muda ili kupisha mvua za Elnino zinazotarajiwa kunyesha mwezi huu wa Oktoba 2023.
Agizo hilo la Mkuu wa Wilaya linakuja kufuatia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwa Wilaya ya Same iliyopo Mkoani Kilimanjaro ni Miongoni mwa Wilaya zilizotabiriwa kuwa na mvua kubwa za Elnino kuanzia wiki ya pili ya mwezi Oktoba 2023.
Amesema kutokana na Utabiri huo tayari Wilaya ya Same imeshaunda Kamati za Maafa za Wilaya (Kamati Elekezi na Kamati ya Wataalam) Kamati za Kata na za Vijiji kwaajili ya kujiandaa kwa njia mbalimbali ili kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hiyo ambapo kwasasa Kamati hizo zinaendelea kutoa elimu kwa Wananchi katika Maeneo mbalimbali.
Ameyataja maeneo ambayo yamekuwa yakiathiriwa na maporomoko ya miamba (landslides) wakati mvua zinapokuwa nyingi katika Wilaya ya Same ni baadhi ya vijiji katika Kata za Myamba,Msindo,Kirangare,Mpinji,Chome na Vunta.
Maeneo ya tambarare ambayo huwa yanaathiriwa na mvua ni maeneo ya Kata za Same,Njoro,Makanya,Hedaru,Ruvu,Maore na Kihurio ambapo maeneo haya hupokea maji yanayotoka katika maeneo ya milimani na hivyo kusababisha mafuriko.
Mkuu wa Wilaya ameziagiza Kamati za maafa za Wilaya,Kata na Vijiji kuendelea kutoa elimu na kuwashauri wananchi kuhama kwa muda katika maeneo hatarishi ili kupisha Mvua zilizotabiriwa kunyesha mwezi Oktoba 2023.
Ameitaka hatua nyingine zinazoendelea kuchukuliwa na Wilaya ili kupunguza athari za Mafuriko ni pamoja na kuzibua mitaro na kuchimba njia za dharura za kupitisha maji katika maeneo yote hatarishi ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi.
Katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko tayari Wilaya imeshaandaa dawa mbalimbali pamoja na kuainisha hospitali,vituo vya afya na zahanati ambazo zipo katika maeneo yanayoonekana kuwa salama ambazo zitakuwa zinatoa huduma kwa wahanga.
"Nawasihi Wananchi wa Wilaya ya Same kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania(TMA) ili kuweza kuchukua hatua kabla madhara hayajatokea
Aidha Wananchi waepuke kukaa chini ya miti, kutembea sehemu hatarishi kama kwenye mikondo ya maji na umeme hasa wakati Mvua ikiwa inanyesha kwani ni hatari kwa maisha yao.
Nitoe angalizo pia kwa wanaotumia vyombo vya Moto waepuke kabisa kupita sehemu ambapo maji ni mengi,waepuke kupita maeneno ambayo maji yamefunika madaraja.
Pia wakati wote wananchi wanapaswa kuwa na akiba ya chakula, fedha, maji, na vifaa vya huduma ya kwanza majumbani mwao kwa kipindi chote cha matarajio ya mvua kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.
Kila mwananchi ahakikishe anakuwa na namba ya simu kiongozi wake katika eneo analoishi iwe ni wa Kijiji au Kata ili aweze kutoa taarifa kunapokuwa na tatizo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.