Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akagua mradi wa bweni na vyumba vinne(4) vya madarasa shule ya sekondari Bombo ambapo vyumba vya madarasa vimekamilika na vimeanza kutumika lakini bweni bado halijakamilika kutokana na wananchi wa eneo husika kutokushiriki ipasavyo katika mradi huo.
Akizungumza na mwalimu mkuu wa shule ya sekondari bombo na diwani wa kata ya Bombo Bi.Shija amewasisitiza na kutoa maagizo kwa mkuu wa shule na mtendaji kata kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa bweni hilo ili kumalizika kwa haraka ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Huu ni muonekano wa bweni katika shule ya Bombo sekondari
Hapo chini ni muonekano wa vyumba vya madarasa ambavyo vimekamilika na vimeanza kutumika
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.