Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anna-Claire Shija akagua mradi wa maji kata ya Hedaru ambapo ametembelea vituo vya maji vinavyoendeshwa na vyombo vya watumia maji ambapo amevipongeza vyombo hivyo kwa jitihada za kuhakiki wananchi wa kata ya Hedaru wanapata huduma ya maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.Sambamba na hilo Bi.Anna-Clare amevitaka vyombo hivyo kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kwa vile vituo visivyopata huduma ya maji wachangie ili waweze kupata huduma ya maji.
Bi.Anna-Claire Shija alikagua mradi wa maji kata ya Vumari kijiji cha Minyala ambapo amemsisitiza mkandatasi wa mradi huo kukamilisha kazi mapema na kukabidhi ili wananchi wa kijiji cha Minyala wapate huduma ya maji.
Bi.Shija alikagua pia mradi wa ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Mabilioni ambapo amebaini kazi isiyo ya kiwango iliyofanywa na mkandarasi wa mradi huo ambapo amemwagiza mhandisi wa ujenzi kumsimamia mkandarasi huyo kufanya marekebisho katika vyoo hivyo na kukabidhi kazi mapema.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.