Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa mkopo usio na riba wenye thamani ya shilingi milioni 100,000,000/= kwa vikundi vipatavyo 26 kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022.Kati ya vikundi hivyo vikundi 7 ni vya vijana ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 31,000,000/=,vikundi 17 vya wanawake ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 62,000,000/= na vikundi 2 vya watu wenye ulemavu ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 7,000,000/=.Katika mkopo huo Halmashauri imechangia Tsh 42,000,000/= kutoka vyanzo vya ndani vya mapato yake na kiasi cha Tsh 58,000,000/= kutoka marejesho ya vikundi.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Same Ndg.Sospeter Magonera Katibu Tawala wa Wilaya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi ameipongeza Halmashauri kwa kutoa mikopo hiyo ambapo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) vilevile amewapongeza kina mama,vijana na watu wenye ulemavu kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.Samia Suluhu Hassan kwamba kina mama,vijana na watu wenye ulemavu wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri.Ndg.Magonera ameviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi na kurejesha ili Halmashauri iweze kutoa tena mikopo.
Vile vile ameviasa vikundi hivyo kutumia na kusimamia mikopo hiyo vizuri kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia lengo la kuongeza kipato kwa kila mwanachama.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg.Rogath Nlula amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na walemavu na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyokusudia na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
Hali kadhalika zoezi la utoaji mikopo limeambatana na utoaji wa baiskeli mjongeo tisa 9 kwa watu wenye ulemavu ambapo zimetolewa msaada kwa Halmashari na Tanzania Cigarate Company(TCC).
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.