Halmashauri ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 96,500,000/= kwa vikundi 32 ambapo vikundi vya wanawake ni 16 waliopata jumla ya shilingi milioni 46,500,000/= na kwa vikundi 15 vya vijana wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 46,500,000/= na kimoja ni cha watu wenye ulemavu kimepata mkopo wenye thamani ya shilingi 3,500,000/=.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Katibu Tawala Wilaya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewataka kina mama na vijana kujituma zaidi kwa kuwa taifa linawatizama wao kwani ndio chachu ya maendeleo kuanzia ngazi ya familia.Ameongeza kuwa kutolewa kwa mikopo hiyo ikabadilishe na kuimarisha hali za kipato cha familia kupitia shughuli mbalimbali za kijasiriamali zinazofanywa na vikundi hivyo.
Mhe.Mgeni rasmi amesisitiza vijana kujiepusha na mambo yasiyofaa ikiwemo uvutaji bangi na madawa ya kulevya,kupoteza muda wao mwingi vijiweni bila kazi ,matukio ya ubakaji na uporaji na badala yake waunde vikundi vya kufanya kazi za kimaendeleo.”Vijana ni taifa la leo,amkeni sasa.”Amesema Katibu Tawala huyo".
Kwa upande wa Katibu wa CCM wilaya ameipongeza Halmashauri ya Same kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi na ahadi ya Mhe.John Pombe Magufuli ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana na walemavu.
Aidha kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ndugu John Nko amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama na vijana na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.