Halmashauri ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 76,000,000/= kwa vikundi 23 ambapo vikundi vya wanawake ni 17 waliopata jumla ya shilingi milioni 56,000,000/= na kwa vikundi 6 vya vijana wamepata mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 20,000,000/= ambavyo vimekidhi sifa za kukopeshwa na hakuna kikundi cha watu wenye ulemavu kilichoomba na kukopeshwa.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Meshack Kingu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewapongeza kina mama na vijana kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.John Magufuli kwamba kina mama na vijana wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.Mhe.Mgeni rasmi amesisitiza vijana kujiepusha na mambo yasiyofaa ikiwemo uvutaji bangi na madawa ya kulevya,kupoteza muda wao mwingi vijiweni bila kazi ,matukio ya ubakaji na uporaji na badala yake waunde vikundi vya kufanya kazi za kimaendeleo.”Vijana ni taifa la leo,amkeni sasa.”Amesema Ndg.Meshack Kingu".
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ameipongeza Halmashauri ya Same kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi na ahadi ya Mhe.John Pombe Magufuli ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana na walemavu.
Aidha kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ndugu Meshack Kingu amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama na vijana na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.