Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 87,000,000/= kwa vikundi 26 ambapo vikundi vya wanawake ni 11 vimepata mkopo wenye thamani ya shilingi 34,800,000/=,vijana vikundi 10 vimepata mkopo wenye thamani ya shilingi 34,800,000/= na watu wenye ulemavu vikundi 5 vimepata mkopo wenye thamani ya shilingi 17,400,000/=.Mikopo hii ni kutokana na asilimia kumi ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri shilingi 36,400,000/= na marejesho ya mikopo ya nyuma shilingi 50,600,000/= ambapo inakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya vikundi,mtu mmoja mmoja na Wilaya kwa ujumla.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stack Senyamule ambaye alikuwa ni mgeni rasmi ameipongeza Halmashauri kwa kutoa mikopo hiyo ambapo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) vilevile amewapongeza kina mama,vijana na watu wenye ulemavu kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la serikali ya awamu ya sita kwamba kina mama na vijana wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kuviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Same Bi.Anastazia Tutuba amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na walemavu na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.