Halmashauri ya Wilaya ya Same imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 100,000,000/= kwa vikundi 23 kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022.Kati ya vikundi hivyo vikundi 9 ni vya vijana ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 40,000,000/=,vikundi 9 vya wanawake ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 40,000,000/= na vikundi 5 vya watu wenye ulemavu ambapo wamepata mkopo wenye thamani ya Tsh 20,000,000/=.Katika mkopo huo Halmashauri imechangia Tsh 14,516,500/= kutoka vyanzo vya ndani vya mapato yake na kiasi cha Tsh 85,483,500/= kutoka marejesho ya vikundi.
Akikabidhi hundi za mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Jonas Mpogolo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi ameipongeza Halmashauri kwa kutoa mikopo hiyo ambapo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) vilevile amewapongeza kina mama,vijana na watu wenye ulemavu kwa kupata fursa hiyo ya kupata mkopo ambapo alisema ni agizo la Mhe.Samia Suluhu Hassan kwamba kina mama,vijana na watu wenye ulemavu wapewe mikopo isiyo na riba kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri.Mhe.Mpogolo ameviasa vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi na kurejesha ili Halmashauri iweze kutoa tena mikopo.
Vile vile ameviasa vikundi hivyo kutumia na kusimamia mikopo hiyo vizuri kwa kufanya kazi wenyewe na sio kuajiri ili kupata faida na fedha ya marejesho."Halmashauri inapopata mapato ndipo jamii itaneemeka kwa mapato hayo".Alisema Mhe.Mpogolo.
Wataalamu wa Halmashauri waagizwa kuviwezesha vikundi kwa kuvishauri kitaalamu na kuvifwatilia vikundi hivyo ili vikue,kuwa na mtandao(networking) ili waweze kusaidia changamoto mbalimbali ya shughuli za vikundi hivyo ikiwa ni pamoja na kuvitafutia masoko.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bi.Anastazia Tutuba amewahakikishia wana Same kwamba Halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama,vijana na walemavu na kuwataka walengwa hao waunge mkono juhudi hizo kwa kufanya kazi kwa bidii,kulinda mapato ya Halmashauri yasipotee,kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyokusudia na kurejesha kwa wakati ili zoezi liwe endelevu.
Bi.Anastazia Tutuba ameviasa vikundi hivyo kutilia maanani elimu na ushauri wanayopewa na wataalamu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.