Waziri wa madini Mhe.Angela Kairuki amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali katika hospitali ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ikiwemo mashine maalumu ya kupimia magonjwa ya moyo (ECG), yenye thamani ya shilingi milioni 137.
Hospitali hiyo itakuwa ya kwanza kwa serikali katika mkoa wa Kilimanjaro kuwa na mashine hiyo maalumu ya kupimia magonjwa ya moyo, ambapo wananchi wa Same na mkoa kwa ujumla wameshauriwa kwenda kupima afya zao. Vifaa vingine vilivyotolewa ni taa kubwa ya upasuaji, taa 2 ndogo za upasuaji, mashuka na foronya 104, vitanda 52, magodoro 52, vifaa vya kufundishia kutembea (magurudumu ) 30, vifaa vya kufundishia kutembea (chuma) 13, clutches vifaa vya kufanyia mazoezi 8, wheel za chair watoto 2, wheel chair za wakubwa 4, screen 5, drip stand 3, vifaa vya kusaidia mikono na miguu iliyoumia, mashine za kupimia pressure 2, miwani 390, plaster 39, dawa za malaria za watoto pakiti 269.
Akikabidhi msaada huo kwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji bwana John Nnko hospitalini hapo Mhe.Kairuki aliongozana na Balozi wa Kuwait nchini Jaseen Al- Najem, alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika sekta ya afya hali iliyosababisha aguswe na kuona umuhimu wa kuchangia vifaa hivyo.
Alisema wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakipatwa na matatizo ya macho na kutakiwa kutumia miwani, lakini kutokana na changamoto za fedha wameshindwa kununua. "Nilipokea taarifa ya kuwepo kwa wagonjwa wengi wa macho wanaohitaji miwani, hivyo nikiwa kama mzaliwa wa Same, nimeamua kutoa miwani 700, kwa leo, nitakabidhi miwani 390 ili ianze kutolewa bure kwa watu wenye uhitaji wa miwani" alisema.
Alitumia fursa hiyo kumuomba Balozi Al-Najem, kusaidia ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la mama na mtoto katika hospitali hiyo, ambapo Balozi aliridhia.
Kwa upande wake, Balozi Al-Najem, aliahidi kutoa vifaa mbalimbali katika hospitali hiyo, ikiwemo kifaa cha benki ya damu.
Balozi Al-Najem alisema kwa sasa, anasubiri kupelekewa mchoro wa jengo la mama na mtoto ili aweze kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stacki, alisema wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta ya afya wilayani humo, hivyo aliomba serikali iwafikirie. Mhe.DC alitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa zahanati, ambapo asilimia 50% ya vijiji 100 vilivyopo katika wilaya hiyo havina zahanati huku ilani ya uchaguzi ya CCM ikitaka kila kijiji kuwa na zahanati ifikapo 2020.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Ndg Isaya Mngulu apongeza utekelezaji wa ilani,awakumbusha watu kuyumia vifaa hivyo kwa kupima afya zao,ahimiza kujiunga na Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Christopher Irira akumbusha uhitaji wa hospitali mpya ya Wilaya.
Aidha Mhe.DC alimshukuru sana Mhe.Kairuki na Balozi Al-Najem kwa mchango wao mkubwa katika hospitali ya wilaya ya Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.