Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mheshimiwa Anne Kilango Malecela amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukipatia kituo cha Afya Myamba gari la wagonjwa.
Akikabidhi gari hilo Mbunge huyo alisema Mheshimiwa Rais imesaidia kutatua changamoto nyingi za wananchi katika Jimbo lake ambapo pamoja na kuwapatia gari la wagonjwa lakini pia wamejengewa vituo vya Afya vitatu.
"Hili gari ninalolikabidhi hapa leo ni mama Samia ndio amesema lije,kwahiyo naomba mumshukuru mama Samia mara kumi zaidi ya mnavyonishukuru mimi maana bila yeye kuamua hili gari lisingefika hapa"alisema.
Alimshukuru pia Rais Samia kwa kuwapatia Shule mpya ya Msingi ya kisasa na Shule mpya ya Sekondari ya Misufini ambapo kwa upande wa kilimo alimshukuru kwa kuwajengea mifereji mikubwa ya umwagiliaji.
Akitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais,mkazi wa Myamba Bw.Daniel Mmbaga alisema gari hilo litakua msaada sana kwa wananchi wa eneo hilo kwani hapo awali wagonjwa walikua wakisafirishwa kwa pikipiki.
"Kumsafirisha mgonjwa kwa pikipiki anapokuwa amezidiwa ni jambo hatari lakini ilikua ndio njia pekee,tunashukuru sana Rais Samia kutupatia,gari hili" alisema.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.