Mbunge wa Same Mashariki Mhe.Anne Kilango Malecela ameiomba Serikali kuwaongezea fedha wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Same ili waweze kujenga daraja la kuunganisha Kata ya Kirangare na Mpinji.
Akizungumza na wananchi wa Kata Kirangare wakati akitambulisha Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Idaruu-Narema yenye urefu wa kilomita 7 Mheshimiwa Kilango alisema Ujenzi wa Barabara hiyo ni muhimu sana kwani utasaidia kuunganisha wananchi wa Kata ya Kirangare na masoko.
Amesema bado wananchi wa Kirangare ambao wanategemea soko la Myamba hawataweza kuvuka upande wa pili hadi daraja hilo litakapokuwa limejengwa.
Akizungumza katika hadhara hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni ameahidi kuwasilisha maombi hayo ya kujengewa daraja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ili aweze kuwasaidia wananchi hao.
"Kwakweli nimejionea uhitaji mkubwa wa wananchi hawa wa kujengewa daraja na nitalifikisha hili kwa Mheshimiwa Rais na Nina imani kubwa kwamba atatuletea fedha za Ujenzi wa daraja hili"amesema Mkuu wa Wilaya.
Kwa Upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Same Mhandisi James Mnene amesema barabara hiyo ya km 7 inayojengwa kwa kiwango cha changarawe inagharimu jumla ya shilingi milioni 395 ambazo no fedha za tozo.
Kuhusu Ujenzi wa daraja la kuunganisha Kata hizo mbili Mhandisi Mnene amesema TARURA itakokotoa gharama za Ujenzi na kuwasilisha TARURA Mkoa kwaajili ya kuomba fedha za Ujenzi maana lina umuhimu mkubwa.
Diwani wa Kata ya Kirangare Mheshimiwa Charles Chaivawa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwakumbuka wananchi wa Kirangare na amewataka wananchi hao kulinda sana miundombinu ya Barabara.
Nae Mwenyekiti wa Kitongoji cha Narema Bw.Anderson Yusuph amesema Ujenzi wa Barabara hiyo utapunguza vifo vya wanawake wajawazito ambao walikuwa wakishindwa kupelekwa hospitali kutokana na miundombinu duni ya Barabara.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.