Kina baba Wilayani Same wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuhudumia familia kwa mahitaji mbalimbali ikiwemo elimu, chakula na malazi ili kupunguza malalamiko yanayowasilishwa Ofisi ya Ustawi wa Jamii.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Idara ya Afya,ustawi wa Jamii na Lishe Wilaya ya Same Dkt. Alex Alexander ambapo alisema malalamiko ya kutelekeza familia yanayopokelewa na Kitengo cha Ustawi wa Jamii ni mengi.
Alisema kwa kipindi cha Miezi mitatu Aprili-Juni 2024 Kitengo cha Ustawi wa Jamii Wilaya ya Same kimepokea jumla ya mashauri 125 ambayo yalisikilizwa pamoja na kutatuliwa,.
“Kwa kipindi cha miezi mitatu tu, migogoro ya familia iliyopokelewa ni 22, waliogoma kutoa matunzo ya watoto ni mashauri 61 na waliotelekeza familia mashauri 42” Alisema Dkt Alex.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Same Bi. Happiness Temu alisema mashauri yote yaliyofika ofisi ya Ustawi wa Jamii yahusuyo matunzo kwa watoto, kutelekeza familia na migogoro ya kifamilia yalitatuliwa kwa kuzingatia miongozo na kanuni na wazazi waliotelekeza familia waliwajibishwa kisheria.
“Kwakweli hali siyo nzuri,wababa wanakimbia familia,wababa wanakwepa majukumu,niwashauri tu wababa watunze familia zao ili kuepuka mkono wa sheria” alisema Bi. Hapiness.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.