Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha siku ya Misitu Duniani ambacho maadhimisho yake Kitaifa yatafanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza akiwa Wilayani Same,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu alisema maadhimisho ya siku ya Msitu Duniani yanatarajiwa kuanza Machi 18 ambapo kutakua na shughuli mbalimbali za kuhamasisha utunzaji wa misitu na kilele chake kitakuwa Machi 21.
"Napenda kuwafahamisha wananchi wa Same kuwa siku ya Misitu Duniani kwa mwaka huu itaadhimishwa Wilayani Same Machi 21 na itaambatana na aonesho ya bidhaa za Misitu pamoja na zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali"alisema Mkuu wa Mkoa.
Akizungumzia ujio huo wa Makamu wa Rais,Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alisema Wilaya imejiandaa vema kuadhimisha siku hiyo ili kukumbushana umuhimu wa kutunza misitu.
"Lengo ni kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa rasilimali za misitu na kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuwa sehemu ya wajibu wa kulinda maeneo ya Hfadhi"alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo yatakaofanyika kwenye Shule ya Sekondari Same ambayo yanabebwa na kaulimbiu isemayo "Misitu na Ubunifu".
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.