Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Same, limeomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 63.42 kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ndani ya wilaya hiyo.B
Bajeti hiyo, ilijadiliwa katika Kikao Maalum cha Bajeti cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Januari 31 kwa ajili ya kujadili na kupitisha mpango wa matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mheshimiwa Yusto Mpande amesema bajeti hiyo imelenga kuboresha na kuimarisha sekta mbalimbali za Maendeleo ndani ya wilaya ya Same ili kuimarisha ustawi wa wananchi wa Same.
Aliwataka madiwani, watendaji pamoja na viongozi wengine Wilayani Same kuhakikisha kuwa mapato yanapatikana ili Halmashauri iweze kutekeleza miradi iliyopitishwa katika bajeti hiyo.
Alisema kipaumbele kwenye Bajeti hiyo ni umaliziaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoishia kwenye maboma ikiwemo ya majengo ya shule, majengo ya miradi ya afya pamoja na mengineyo ili walengwa waweze kunufaika nayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Same Bi. Upendo Wella amepongeza namna bajeti hiyo ilivyowasilishwa na kuwaomba madiwani pamoja na watendaji kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato kutokana na uwepo wa mahitaji mengi zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Diwani wa Kata ya Makanya, Damari Kingalu amesema kuwa bajeti hiyo imelenga zaidi kwenye miradi inayoigusa jamii moja kwa moja ikiwemo elimu, afya na usafirishaji huku akiwasisitiza wananchi kushiriki katika shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
@ortamisemi
@maelezonews
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.