Mkuu wa Wilaya ya Same, Mheshimiwa Kasilda Mgeni, amewataka Maafisa Utumishi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa Watumishi wanapata stahili zao za kiutumishi kwa wakati ili kupunguza malalamiko yanayotokana na Watumishi wakiwemo walimu kucheleweshewa stahili zao.
Akizungumza katika kliniki ya kutatua changamoto za walimu (Samia Teacher's Mobile Clinic) iliyowakutanisha walimu kutoka Wilaya za Mwanga na Same, Mhe. Kasilda ameeleza kuwa changamoto nyingi wanazokutana nazo walimu zinaathiri utendaji wao wa kazi, hivyo kupunguza ubunifu na ufanisi.
"Walimu wanapokumbwa na changamoto katika upatikanaji wa stahili zao na utendaji wao lazima ushuke hakutakuwa na ubunifu, na hali hii inaathiri ubora wa elimu"amesema.
Baadhi ya changamoto ambazo walimu waliwasilisha ni pamoja na kucheleweshwa kupandishwa madaraja, kubadilishiwa miundo baada ya kujiendeleza, malimbikizo ya mishahara, madai ya muda mrefu ya stahiki za uhamisho pamoja na madai ya kustaafu.
Timu inayojumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakishirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) imefika Wilayani Same na kusikiliza kero mbalimbali za walimu na kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Suleiman Ikomba ameishukuru Serikali kwa kuwa sikivu na kuunda klinik hiyo ambayo utasaidia kutatua changamoto za walimu.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.