Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Mheshimiwa Yusto Mapande amekabidhi pikipiki kwa maafisa Mifugo saba Wilayani humo ili kurahisisha utendaji wao wa kazi ya kuhudumia mifugo.
Akizungumza wakati akikabidhi pikipiki hizo Januari 29 mwaka huu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Yusto Mapande amewataka maafisa Mifugo hao kutumia vyombo hivyo kuwapatia wananchi huduma ili wananchi waweze kuona mafanikio ya serikali yao.
“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia pikipiki hizi kwani kutokana na jiografia ya Wilaya ya Same zitasaidia sana kurahisisha utoaji wa huduma za mifugo kwa wananchi wetu”alisema Mheshimiwa Mapande
Mwenyekiti huyo amewataka maafisa Mifugo hao kuhakikisha wanatunza pikipiki hizo kwani ni mali ya Serikali na wahakikishe wanazitumia kwa malengo tarajiwa na sio vinginevyo kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanafikishiwa huduma wanazohitaji.
“Tunawapa pikipiki hizi leo,naomba nendeni mkatoe huduma iliyo bora kwa wananchi wetu tusifanye matumizi mabaya ya mali hizi za serikali mmepatiwa kwa lengo mahususi la kutoa huduma kwa wananchi wetu na si vingine nendeni sasa mkakutane na wafugaji na kuwasaidia”alisema
Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilayani Same Dkt. Cainan Kiswaga amesema kulingana na jografia ya maeneo mengi ya Wilaya ya Same kumekuwa na changamoto kubwa ya kufikika kwenye maeneo mbalimbali kutokana na ukubwa wa Kata.
“Tunaishukuru sana Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutuletea pikipiki hizi kwani zitasaidia sana kwa maafisa Mifugo wetu kuwafikia wafugaji wengi na kwa wakati “Alisema Dkt.Kiswaga
Nao baadhi ya maafisa Mifugo waliopatiwa pikikipiki hizo akiwemo Bw Evarest Massawe kutoka Kata ya Ndungu na Bi. Ambisile Myale kutoka Kata ya Mabilioni wamesema pikipiki hizo zitasaidia kuondoa malalamiko kwa wafugaji kwani watakuwa wanawafikia kwa wakati na kutoa huduma.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.