Kufuatia kufunguliwa kwa dirisha la mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Wilaya ya Same imetoa mafunzo kwa maafisa Maendeleo ya Jamii zaidi ya 30 ngazi ya Kata juu ya utaratibu wa kuwasilisha maombi kupitia mfumo wa Wezesha Portal.
Akitoa mafunzo kwa maafisa hao Afisa Maendeleo Wilaya ya Same Bw. Charles Anatoly alisema kwasasa mfumo wa unaotumika kupokea maombi ni mfumo ulioboreshwa ambao unawezesha mchakato wa upatikanaji wa mkopo kwa haraka.
Alisema Mfumo huo ujulikanao kama Wezesha Portal umeshafanyiwa majaribio na umeonesha mafanikio hivyo maafisa Maendeleo Kata wamepewa elimu ili waweze kuwasaidia wanavikundi kuomba mkopo kwenye mfumo.
”Serikali imeboresha mfumo wa uombaji wa mikopo ili kuviwezesha Vikundi kuomba mikopo kwa urahisi na kuharakisha mchakato wa wao kupata mikopo”alisema Bw.Anatoly
Maombi ya mikopo ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu yameanza kupokelewa kupitia mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz na mwisho wa kupokea maombi ni Oktoba 10,2024.
Halamshauri ya Wilaya ya Same ina vikundi zaidi ya 100 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambavyo vimesajiliwa na vina sifa ya kuomba mikopo hiyo.
“Mikopo ya awamu hii itatolewa kwa vikundi ambavyo havidaiwi na halmashauri,kama kikundi kinajua kina deni la nyuma kilipe kwanza deni ndio kiombe mkopo mwingine”alisema Bw. Anatoly
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.