Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imewapatia Maafisa Kilimo wa Wilayani Same vishikwambi 39 ili kuwezesha taarifa mbalimbali za kilimo kutolewa kwa wakati kwa njia ya mtandao na kuwezesha maafisa kilimo kuingia kwenye mifumo mbalimbali kwaajili ya kutoa na kupokea taarifa zitakazowezesha uboreshaji wa kilimo.
Akikabidhi vishkwambi hivyo ,Kaimu Afisa Tawala Wilaya ya Same Bw. Sixbert Sarmett alisema sekta ya kilimo ni kubwa na imebeba hatma ya watanzania hivyo amewataka maafisa kilimo kuhakikisha kuwa wanatumia zana hizo vizuri ili kuboresha kilimo.
"Leo tumewakabidhi vitendea kazi,tunatambua shughuli nyingi za serikali zinatumia mifumo hivyo mkavitumie vyema vishkwambi hivi kutatua changamoito za kilimo na kuvitunza viweze kudumu "Alisema Bw. Sarmett
Afisa Kilimo Dkt. Cainan Kiswaga alisema kuna jumla ya vishikwambi 39 ambavyo vimeletwa kwa ajili ya maafisa Kilimo wote katika kata zote ambavyo vitatumika katika kuhifadhi taarifa mbalimbali zinazohusu sekta hii ya kilimo.
"Tunaamini kuwa maafisa kilimo wote waliopata vishikwambi hivi itawawia rahisi kutekeleza majukumu yao hasa ya ukusanyaji na utoaji wa taarifa sahihi kwa wakati” alisema Dkt.Cainan
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.