Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Edward Mpogolo amewataka wanaSame kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamuhuri kama chachu ya mabadiliko kiuchumi,kifikra,kimaendeleo,kiafya na kielimu,aliyazungumza hayo alipokuwa akitembelea maonesho ya mabanda ya taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali ambapo maonesho hayo yalifanyika katika eneo la viwanja vya stendi ya mabasi Same.
Taasisi zilizofanya maonesho hayo ni TANESCO,Magereza,Polisi dawati la jinsia na watoto,NMB Banki,TCB Bank,Mwanga Hakika Bank,RUWASA,SAUWASA,Same Kaya Saccos,Same Teachers Saccos,Mkomazi,Ofisi ya mganga mkuu kitengo cha utoaji chanjo ya Uviko 19 na Upimaji virusi vya UKIMWI,kikundi cha Kazi Iendelee,kikundi cha uchenjuaji madini ya kopa,TRA,TAKUKURU,M-POWER na kikundi cha ujasiriamali wa kutengeneza Lishe.
Vikundi vyote hivyo vilitunukiwa vyeti vya shukrani na appreciation na Mhe.Mpogolo.
Hapa ni katika tukio la kukabidhi cheti kwa wataalamu wa TANESCO ambapo Mhe Mkuu wa Wilaya amewapongeza kwa kufikisha huduma kwa takribani wilaya yote ya Same na kuwataka kufikisha umeme katika maeneo yote hata ambayo hayajajengwa
Hapa Mhe.Mpogolo akikabidhi cheti kwa banda la ofisi ya TAKUKURU
Hapa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya akikabidhi vyeti vya shukrani kwa taasisi
Hapa Mhe.Mpogolo akipokea zawadi
Hapa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya akiwa anaendelea kutoa vyeti vya shukrani
Baada ya kutembelea mabanda hayo kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki katika viwanja vya kwasakwasa kati ya kurugenzi FC na boma FC ambapo boma FC waliibuka kidedea kwa kupata ushindi wa magoli sita 6 hii yote ni katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamuhuri
Hapa Mhe.Mpogolo,Bi.Annastazia Tutuba,Katibu wa CCM wilaya Mhe.Hamisa na Katibu Tawala Wilaya Ndg.Magonera wakiwa wanafwatilia mechi.
Hali kadhalika katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamuhuri mamlaka ya mji mdogo Same kwa kushirikiana na benki ya NMB Same,wafanyabiashara wa soko kuu na viongozi wa mtaa wa sokoni wamefanya usafi wa eneo zima la soko kuu Same kama inavyoonekana hapo chini.
Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamuhuri tufanye kazi kwa bidii na uadilifu ili kuijenga Same yetu na Taifa kwa ujumla.
Kazi Iendelee.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.