Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mnghwira aliyekuwa mgeni rasmi katika siku ya mazingira duniani iliyoadhimishwa kimkoa wilayani Same kata ya Ruvu kijiji cha Ruvu jiungeni katika kambi ya wahanga wa mafuriko Loresho ambapo kulikuwa na zoezi la upandaji miti lililozinduliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dr.Regnald Mengi,upigaji chapa mifugo,maonesho ya bidhaa mbalimbali katika vibanda na upimaji afya bure.
Akihutubia wananchi katika kambi ya wahanga Loresho Mhe.Mkuu wa Mkoa ametoa pole kwa wahanga hao na kuwatia moyo kwamba hawana budi kukubaliana na hali halisi na kwamba maisha lazima yaendelee.Akizungumza katika maadhimisho hayo ya siku ya mazingira amewaasa wananchi kuyatunza mazingira ili kuepukana na athari zinazojitokeza kama mafuriko,ukamen.k.
Aidha Mhe.Anna Mnghwira amewashukuru wadau mbalimbali na taasisi za kidini kwa kutoa misaada ya vyakula,mavazi,malazi,fedha taslimu na vitu mbalimbali kama sabuni,maturubai.Kipekee kabisa Mhe.Mkuu wa Mkoa alitoa shukrani za dhati kwa mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr.Regnald Mengi kwa msaada mkubwa alioutoa wa vitu na fedha taslimu.
Mwisho Mhe.Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kwa Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya kuwashawishi wananchi kuanzisha vitalu vya miche ya miti,kupanda miti na kurudia zoezi la kuhakiki mifugo.
Bofya HAPA kusikiliza hotuba ya Mhe.Anna Mnghwira aliyoitoa siku ya mazingira duniani iliyoadhimishwa kimkoa wilayani Same kata ya Ruvu.
Bofya HAPA kusikiliza nasaha za wadau mbalimbali na taasisi za kidini zilizotolewa siku ya mazingira duniani wilayani Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.