• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Same District Council
Same District Council

Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Same

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idaraya Elimu Sekondari
      • Rasili Mali Watu na Utawala
      • Ardhi Maliasili na Utalii
      • Fedha Na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Kazi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi.
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo Cha TEHAMA
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo Cha Uchaguzi
      • Kitengo Cha Manunuzi
      • Kitengo Cha Sheria
    • Kata
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Mipango
      • Elimu,Afya na Maji
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
      • TAMKO LA VIONGOZI WA UMMA KUHUSU RASILIMALI NA MADENI
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Stoo Ya Picha

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE AIPONGEZA SAME KWA UBORA WA MIRADI

Posted on: June 21st, 2023

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2023 Ndg. Abdallah Shaib Kaim ameeleza kuridhishwa na Ubora wa Miradi saba  ya Maendeleo  aliyoitembelea katika Wilaya ya Same wakati Mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa Wilayani humo.

Mwenge wa Uhuru uliwasili na kukimbizwa katika Wilaya ya Same Juni 20 mwaka huu ambapo Mwenge huo ulifikia Miradi saba  ikiwemo Miradi ya Afya,Maji,Elimu,Mazingira, Barabara na Ujasiriamali yenye thamani ya shilingi Bil.3.68.

Akizungumza baada ya kukagua Miradi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg.Abdallah alisema ameridhishwa sana na Ubora wa Miradi na mpangilio mzuri wa Nyaraka za Miradi yote iliyofikiwa na Mbio za Mwenge.

“Tumefanya Ukaguzi wa kina wa Miradi na Nyaraka,tumejiridhisha na Ubora na thamani ya fedha,niwapongeze sana Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi kwa usimamizi makini wa Miradi” alisema Ndg.Abdallah

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru Mkoani Kilimanjaro ukitokea Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Nurdin Babu alisema ukiwa Mkoani Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru utafikia Miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bil.30.3 na ulianzwa kukimbizwa katika Wilaya ya Same.

Baada ya Mkuu wa Mkoa kupokea Mwenge wa Uhuru aliukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mshikizi Bw.Amir Mkalipa kwaajili ya kuanza kuukimbiza katika Wilaya ya Same.

“Katika Wilaya ya Same tutakimbiza Mwenge wa Uhuru kwenye umbali wa  Kilomita 102 na utafikia Miradi ya Maendeleo saba yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.86”alisema Bw.Amir

Ukiwa Wilayani Same Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa kona korofi  za barabara ya Hedaru-Vunta –Myamba(mita 810)wenye thamani ya shilingi milioni 655.5.

Mwenge pia ulizindua Madarasa Mawili katika shule ya Sekondari Chauka yenye yaliyojengwa kwa thamani ya shilingi mil.42.6 ambazo ni mgawo wa fedha za tozo,katika shule ya Chauka Mwenge Ulizindua pia Klabu ya Wapinga Rushwa.

Mwenge pia uliweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Zahanati ya Saweni ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 95,Mwenge pia ulitembelea Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Wilaya ya Same ambayo katika awamu ya kwanza ujenzi wake umegharimu Shilingi bilioni 2.

Miradi mingine iliyofikiwa na Mwenge Wilayani Same ni  Mradi wa Maji Mwembe wenye thamani ya shilingi 662.1 ambao ulizinduliwa pia Mwenge ulizindua Kitalu cha Miti TFS chenye thamani ya shilingi Mil.112.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 31, 2021
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI May 06, 2025
  • Siku ya kufanya usafi mwezi Septemba September 08, 2021
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2020 August 21, 2020
  • Tazama Vyote

Habari Za Sasa

  • WACHIMBA MADINI SAME WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA

    May 19, 2025
  • SAME YAPANIA KUONGEZA UZALISHAJI WA MKONGE

    May 05, 2025
  • SAME YAPANIA KUONGEZA UZALISHAJI WA MKONGE

    May 05, 2025
  • SAME YAOMBA WIZARA YA KILIMO KUIPATAIA MICHE YA PARACHICHI

    May 01, 2025
  • Tazama Vyote

Video

KARIBU MWENGE WA UHURU SAME KILIMANJARO 2022
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Forms And Templates
  • Galleys
  • News
  • Events
  • Strategic Plan
  • Reports
  • Acts
  • Malalamiko

Viunganishi Vyenye Uhusiano

  • PO-Ralg
  • PO-Psm
  • e-Government Agency
  • Kilimanjaro Region
  • Employment
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Watembeleaji

free HitCounter

Ramani Ya Wilaya

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.