Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Rosemary Stacki ameungana na maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Same cha tarehe 8/9 mwezi Februari kilichopitisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Katika bajeti hiyo ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na matumizi ya kawaida ya idara na vitengo pamoja na miradi ya maendeleo.Akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC)leo tarehe 27.02.2018 Mhe.Rosemary amewataka watumishi wa Wilaya ya Same kuwajibika ipasavyo kila mmoja kwa nafasi yake ili kufikia malengo ya mafanikio kiwilaya sambamba na kauli mbiu ya Mhe.Raisi John P.Magufuli ya “hapa kazi tu”
Wakati huohuo amesisitiza wakuu wa idara wanaohusika na ufwatiliaji wa mashine za kukusanyia mapato kufawatilia kwa umakini zaidi ili kuongeza mapato wilayani Same.
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.