Wananchi wa Kijiji cha Duma kwenye Kata ya Msindo Wilayani Same wameiomba Serikali kuwajengea Shule nyingine ya Sekondari kwenye Kata hiyo kwani iliyopo sasa ipo umbali wa zaidi ya kilomita sita toka kilipo Kijiji hicho.
Akizungumza kwenye mkutano uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni,Mkazi wa Duma Bw.Harison Mrutu aliomba Serikali kuwajengea Shule mpya ya Sekondari kwani Shule ya Kata (Madiveni) wanayoitegemea ipo mbali toka kilipo Kijiji cha Duma.
"Tunaomba Sana tujengewe Sekondari nyingine kwani Sekondari ya Madiveni tunayoitegemea kwasasa ipo mbali Sana ambapo inawalazimu watoto kutembea zaidi ya kilomita 12 kwa siku kwenda na kurudi Shule"alisema Mzee Harrison.
Akijibu maombi hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Bw.Jimson Mhagama aliyekuja ameambatana na Mkuu wa Wilaya,aliwataka wananchi hao kuanza kuandaa eneo la ujenzi na kuleta maombi rasmi ambayo yatapitishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata ili Serikali Ione namna bora ya kuwajengea Shule.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alisema kwa sasa Serikali inakamilisha Ujenzi wa Bweni kwenye Shule ya Sekondari Madiveni ili Bweni hilo lowe msaada kwa wanafunzi wanaotoka mbali wakati mchakato wa kujenga Shule nyingine ukiendelewa.
Mheshimiwa Kasilda amefanya ziara ya kikazi kwenye Kata ya Msindo Wilayani Same ambapo alitembelea Kijiji cha Duma na kupata fursa ya kuzungumza na wananchi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.