Timu ya Kampeni ya 'Mtu ni Afya' kutoka Wizara ya Afya imefika Wilayani Same na kutambulisha Kampeni hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni.
Muendeshaji wa Kampeni hiyo Msanii Mrisho Mpoto amesema Kampeni hiyo ina lengo la kuelimisha wananchi kuepuka tabia zinazoleta madhara kwenye Afya.
"Kampeni hii inalenga kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kunawa mikono,umuhimu wa kusafisha mazingira yanayowazunguka,umuhimu wa kula mlo kamili,umuhimu wakufanya mazoezi "amesema.
Amesema Kampeni hiyo inajumuisha pia elimu kuhusu hedhi salama kwa watoto wa kike.
Akiwakaribisha Wilayani Same,Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Kasilda Mgeni alisema timu hiyo imefika wakati muafaka ili kuunga mkono juhudi za Serikali Wilayani humo za kutoa Elimu ya Afya.
"Kama Wilaya tunachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na Afya njema ambapo suala la kunawa mikono kwa maji tiririka limekuwa likisisitizwa huku Wilaya ikitoa Elimu ya lishe kwa mama wajawazito na wanafunzi mashuleni"alisema.
Alisema katika kuzingatia hedhi salama Wanawake Wilayani humo waligawa taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule nne za Sekondari kama maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Timu ya Kampeni ya Mtu ni Afya-"Fanya Kweli,usibaki nyuma" itafanya Kampeni Machi 11 na 12 ,2025 kwenye Kata za Hedaru na Same.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.