Timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) Wilaya ya Same ikiongozwa na Mratibu wa Kampeni hiyo Wilaya Bi.Happiness Rhobi imetoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani na kwa wananchi wa Kijiji cha Kadando Kata ya Maore
Wananchi wa Same wanaendelea kunufaika na elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, masuala ya ndoa na talaka,masuala ya ardhi,Elimu ya kusajili vizazi na vifo.
Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia ilianza kutolewa Wilayani Same Januari 30,2025 na itakamilika Februari 8 ,2025.
Mratibu wa Wilaya Bi.Happiness Rhobi alisema Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia(MSLAC) ilianza mwaka 2023 hapa nchini na inategemea kukamilika mwaka 2026.
Alisema Kampeni imeshafikia mikoa 16 na Kilimanjaro ni Mkoa wa 17 ambapo kwenye Wilaya ya Same Utekelezaji unafanyika kwenye Kata kumi.
Kwa Wilaya ya Same alisema Kata zitakazofikiwa kuwa ni Vumari,Kisiwani,Makanya,Mabilioni,Ruvu,Myamba, Hedaru ,Ndungu, Mwembe na Maore
Alisema Lengo la Kampeni ya Mama Samia Legal Aid ni kutoa Elimu kwa Jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo:-
Elimu ya Masuala ya Ardhi
Elimu kuhusu masuala ya Ndoa na Talaka
Elimu ya Mirathi na umuhimu wa kuandika Mirathi.
Alisema Kampeni pia imelenga kuwapa msaada wa kisheria bure wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria.
Alisema matarajio makubwa ya kutoa Msaada wa Kisheria wa Mama Samia ni kupungua
au kumalizika kabisa kwa migogoro na kuwezesha wananchi kupata haki.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.