Kamati ya fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Same imetembelea na kukagua Miradi ya Ujenzi wa mabweni matatu kwenye Shule za Sekondari za Kibacha na Makanya.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emanuel Mhina alieleza kuridhishwa na Maendeleo ya Ujenzi wa mabweni hayo ambayo yapo kwenye hatua ya umaliziaji.
Akizungumza baada ya kutembelea mabweni mawili yanayojengwa kwenye Shule ya Sekondari Kibacha,mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mathias Mrita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Same aliwapongeza walimu kwa usimamizi nzuri wa Ujenzi huo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mhina alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Same fedha za kuwezesha Miradi hiyo.
Akitoa taarifa ya Ujenzi wa mabweni mawili kwenye Shule ya Sekondari Kibacha, Katibu wa Kamati ya Ujenzi Mwl.Daudi Makorenda alisema katika bweni la kwanza walipokea mili.80 toka mpango wa EP4R na baadae wakaongezewa mil.20 toka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Alisema kwa bweni la pili wamepokea Shilingi mil.100.9 Fedha ambazo zimetumika kujenga bweni la pili na kumalizia Ujenzi wa bweni la kwanza ambapo alisema mabweni yote mawili yenye uwezo WA kuchukua wanafunzi 160 yanatarajia kukamilika mapema mwezi Septemba,2024.
Akitoa taarifa ya Ujenzi wa bweni la wavulana kwenye Shule ya Sekondari Makanya,Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Bernad Mgaya alisema awali Shule hiyo ilipatiwa mil.80 kwaajili ya Ujenzi wa bweni lakini hazikutosha hivyo wameongezewa mil.80.5 toka Serikali kuu na ndizo zinazotumika kukamilisha bweni hilo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.