Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Ya Wilaya ya Same Ndg.John Nko ameambatana na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo ambao ni Mganga Mkuu wa wilaya Dr.Andrew Godfrey,Afisa Mipango wilaya Ndg.Simon Vedustus,Mhandisi wa Ujenzi wilaya Eng.Jonathan Nzaro na Afisa Ugavi wilaya Ndg.Thomas Kiria katika kukagua mradi wa maendeleo wa vituo vya afya Ndungu na Shengena ambapo mafundi wasisitizwa kufanya kazi kwa bidii,ufanisi na umakini ili majengo hayo kuwa imara na yenye viwango na ubora.
Mafundi wasisitizwa kufanya kazi mchana na usiku ili majengo hayo kukamilika kabla ya tarehe ya mwisho iliyopangwa.
Yafuatayo ni muonekano wa majengo ya kituo cha afya Ndungu ambapo kuna jengo la maabara,jengo la upasuaji(Theater),wodi ya wazazi na jengo la kuhifadhia maiti(motuary).
Yafuatayo ni muonekano wa majengo ya kituo cha afya Shengena ambapo kuna jengo la maabara,jengo la upasuaji(Theater) na wodi ya wazazi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.