Halmashauri ya Wilaya ya Same imeungana na taasisi zingine za serikali na zisizo za serikali katika kuadhimisha siku ya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) duniani leo tarehe 01 Desemba 2018 ambapo maadhimisho hayo yameadhimishwa kimkoa wilayani Same katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi mjini Same.Mkuu wa wilaya ya Same Mhe.Rosemary Senyamule alimwakilisha mgeni rasmi Mhe.Dkt Anna Mghwira ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza katika hotuba yake Mhe.Rosemary Senyamule amewataka wananchi kuendelea kujitokeza na kupima afya zao ili kufikia lengo la 90/90/90 ifikapo 2020.
Vilevile kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe.Senyamule amewaagiza wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huu (ARV) zinakuwepo bila kukosa katika vituo vyote vya afya.
Tukio hilo limehudhuriwa na wanafunzi wa chuo cha uuguzi,wataalam mbalimbali,wadau wa masuala ya kupambana na ugonjwa wa UKIMWI na mamia ya wananchi wa kata ya Same.Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka 2018 ni “Jua hali yako,Pima ,Jitambue,Ishi”. UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Sherehe hizo zimepambwa na shamrashamra nyingi ikiwemo ushairi,nyimbo na makala. Shamrashamra hizo zimesheheni elimu, jumbe nzito,makatazo na maonyo makali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu ugonjwa hatari wa UKIMWI.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.