Ubalozi wa Japan umetoa Tsh.Mil.281.3 kufadhili Ujenzi wa Zahanati ya Malindi kwenye Kata ya Suji Wilayani Same.
Fedha hizo zimefanikisha Ujenzi wa Zahanati hiyo pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh.Mil.30.
Kamati Fedha,Uongozi na Mipango ilitembelea Zahanati hiyo na kujionea matumizi ya fedha hizo.
Akizungumzia kwenye ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mhe.Yusto Mapande alieleza kuridhishwa na ujenzi huo.
"Tuwashukuru sana wenzetu wa Japan kwa msaada huu kwani unasaidia zaidi ya wananchi zaidi ya 3,000 wa Kijiji cha Malindi na vijiji vya jirani"alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Diwani Kata hiyo Mhe.Edith Banzi alisema wananchi wa Kata hiyo wamechangia Shilingi milioni 113 ikiwa ni utoaji wa eneo la ujenzi na kujenga nyumba moja ya daktari.
"Kwa nguvu za wananchi pia tunarajia kujenga nyumba nyingine ya 2 in 1 ya wauguzi na tayari tumeshafyatua tofali na kununua baadhi ya vifaa"alisema Diwani Banzi.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.