Serikali imelazimika kutumia Helkopta kutafuta makundi ya Tembo na wanyama wengine waharibufu waliozagaa katika vijiji 25 vya Wilaya ya Same na kuwarejesha katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi.
Zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohamed Mchengerwa alilotoa hivi karibuni alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika wilaya hiyo ya Same ambapo aliagiza mamlaka ya hifadhi za Taifa TANAPA kupeleka Helkopta katika Wilaya hiyo kusaidia zoezi la kuondoa makundi ya Tembo yaliyozagaa katika maeneo mbalimbali na kuwarejesha katika hifadhi ya Mkomazi.
Oparesheni hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano baina ya taasisi nne zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Same na wananchi wenyeji ambao wanasaidia kuainisha maeneo walipo Tembo.
Akizungumzia utekelezaji wa Oparesheni hiyo, Mkuu wa hifadhi ya Taifa Mkomazi, amishna Msaidizi wa uhifadhi Emmanuel Moirana amesema kwa siku ya kwanza jumla ya makundi matano ya Tembo yamerejeshwa hifadhini.
"Mkakati uliopo ni kuendelea na zoezi ili kuondoa changamoto ya mara kwa mara kuripotiwa makundi ya Tembo kuonekana maeneo ya nje ya hifadhi ambao wanaathiri shughuli za kibinadam"alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.Kasilda Mgeni amepongeza jitihada hizo za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uharaka wa kutekeleza ahadi ya kuondoa Tembo hao hivyo kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Same walioshiriki katika Oparesheni hiyo wamesema kuna idadi kubwa ya Tembo ambao wametoka kabisa kwenye maeneo ya hifadhi na kufanya makazi ya kudumu kwenye maeneo ya vijiji, hali ambayo imesababisha baadhi yao hasa wakulima mwaka huu kukosa kabisa mazao kwani yameliwa na Tembo.
The Way Through Mkomazi Nationa Park or District Hospital(Kibacha Rd)
Sanduku La Posta: P.O.Box 138
Simu ya mezani: +255 27 2758034
Simu Ya Mkononi: +255 717657681
Email: ded@samedc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Same.Haki zote zimehifadhiwa.